October 17, 2016

MWAMUZI HUYU PIA ALIPIGWA MKWAKWANI WAKATI WA MECHI YA YANGA VS COASTAL UNION

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema linasubiri ripoti ili kamati ya saa 72 ikae na kuamua kuhusiana na mwamuzi aliyepigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, jana.

Mwamuzi huyo aitwaye Mkombozi, alipigwa kama mwizi mara baada ya mechi ya daraja la kwanza kati ya Coastal Union waliokuwa wenyeji wa KMC FC ya Dar es Salaam.

Wageni KMC FC walishinda kwa mabao 3-2, wakiwa wamepata bao la ushindi ‘jioni’ kabisa.

Hali hiyo iliwaudhi mashabiki wa Coastal Union ambao walimpiga kama mwizi huku askari mmoja tu akipambana vilivyo kuhakikisha anamuokoa.

Pamoja na kumlalamikia mwamuzi, uwanja wa Mkwakwani umekuwa kinara cha waamuzi kupigwa.


Waamuzi wamepigwa katika michuano ya Ligi Kuu Bara, msimu uliopita na mwisho timu zote tatu za Tanga, Coastal Union, African Sports na Mgambo Shooting zilizokuwa zinashiriki Ligi Kuu Bara, zikateremka daraja na kuushangaza umma wa wapenda soka nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV