October 15, 2016


Mtanzania Mbwana Samatta ameendelea kuwa msaada mkubwa wa timu yake ya KRC Genk baada ya kuisaidia kupata sare ya mabao 2-2 katika mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Royal Excel Mouscron.

Msaada alioutoa Samatta, safari hii ni pasi ya bao la kusawazisha ikiwa ni dakika chache baada ya kuingia akitokea ‘ubaoni’.

KARELIS ALIYEPIGA BAO ZOTE MBILI, MOJA AKIMALIZIA PASI YA SAMATTA.
Genk ikiwa ugenini, ilijikuta ikifungwa bao katika dakika ya 2 kupitia Trezeguet na Nikos Karelis akasawazisha katika dakika ya 32 na wenyeji wakaongeza kupitia Valentine Viola dakika ya 42 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko Royal wakiongoza kwa 2-1.

Kipindi cha pili kilionekana kuwa kigumu kwa Genk hadi alipoingia Samatta katika dakika ya 67 akichukua nafasi ya Leon Bailey rais wa Jamaica.

Samatta alitoa pasi hiyo ya bao katika dakika ya 78 na Karelis akaimalizia kwa kufunga bao safi la kusawazisha kwa Genk.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic