Kocha Hans van der Pluijm amebwaga manyanga baada ya kuona Yanga wanamletea dharau kama alivyosema yeye.
Walimleta nchini Kocha George Lwandamina kutoka Zambia wakati wakijua yeye yupo na anaendelea na kazi.
Kikubwa ambacho SALEHJEMBE imegungua, Pluijm raia wa Uholanzi alikuja nchini akiwa amevaa shati la rangi nyeupe lenye michirizi ya rangi nyekundu na bluu na ndilo alilivaa siku ya mwisho kuonana na wachezaji wa Yanga alipokwenda kuwaaga kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road.
Pluijm alirejea nchini akiwa amevaa shati hilo baada ya Yanga kumuita tena akitokea Ghana anakoshi na familia yake, hiyo ikiwa ni mara ya pili kurejea nchini na kuinoa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment