Ukipata nafasi ya kukaa na kuzungumza na Nassor Bin Slum, atakuwa enzi zake alikuwa hatari sana. Akiwa na mpira, unaweza kumfananisha na Zinedine Zidane wa zamani.
Anasema angeamua kuendelea na soka, angekuwa mbali. Kwa kuwa kweli “anajua”.
Lakini inakuwa vigumu kupata uhakika kwa kuwa hajaonekana katika anga za juu kisoka. Ingawa takwimu zinaonyesha Watanzania wengi wanajua soka, lakini mwelekeo wa maisha, uliwabadilisha.
Picha tatu, akiichezea Team Ismail katika mechi dhidi ya Team Dizzo katika tamasha la Kandanda Day, jana, zinaonyesha ‘kiana’ Bin Slum anaujua.
Picha hizi tatu zinaonyesha matukio matatu tofauti. Moja, akitafuta nafasi, mbili akimiliki mpira na tatu akiachia shuti. Hivi huyu jamaa anajua kweli, au mbwembwe tu? acha tuendelee kumfuatilia.
0 COMMENTS:
Post a Comment