October 26, 2016


Mshambuliaji Thomas Ulimwengu amesema atafanya mazoezi gym pekee na si pamoja na Azam FC.

Awali, Meneja wake, Jamal Kisongo alisema Ulimwengu ni majeruhi, akipona ataungana na Azam FC kwa ajili ya kujiweka fiti wakati akisubiri ishu yake ya kupata timu Ulaya.

Lakini Ulimwengu amesema hawezi kufanya mazoezi na timu ambayo iko Ligi kuu.

“Siwezi kabisa, nitafanya mazoezi gym tu ili kujiweka fiti,” alisema.

Ulimwengu yuko jijini Dar es Salaam akisubiri suala la kwenda kucheza Ulaya na Kisongo amesema kuna timu zinamhitaji katika nchi mbalimbali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV