October 27, 2016




Kocha wa Stand United, Athumani Bilal amesema wanajua ugumu wa mechi dhidi ya Simba, lakini wanachotaka ni pointi tatu.

SImba itacheza na Stand United Novemba 6 ikiwa ni siku chache baada ya kucheza na Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Stand United ndiye timu pekee ambayo imeshinda dhidi ya vigogo ambao ni Yanga na Azam FC na wote imewafunga kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Bilo ambaye ni beki wa zamani wa Shinyanga Shooting amesema wanajua Simba wana timu mzuri lakini wao wana kikosi bora na wata[ata nafasi zaidi ya kuiona ikicheza na Mwadui.

“Lazima iwe mechi ngumu, hata sisi tunalijua hilo. Lakini kikubwa kwetu tukiwa hapa nyumbani tunachotaka ni pointi tatu,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic