November 29, 2016
Ndege imeanguka karibu na mji wa Medellin nchini Colombia ikiwa imebeba abiria 72 kati yao wakiwa ni wachezaji wa timu ya daraja la kwanza nchini Brazil ya Sudamericana.

Imeelezwa kwamba watu nane tu wameokoka na bado haijajulikana ni akina nani kwa kuwa ndege hiyo imeanguka katika sehemu mbaya ambayo ilinyesha mvua kubwa ile mbaya.Meya wa jiji la Medellin, Federico Gutierrez amethibitisha kudondoka kwa ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria hao 72 pamoja na wafanyakazi wanane.

Kikosi cha Sudamericana kutoka Kusini mwa Brazil kilikuwa katika ndege hiyo ya Lamia yenye makao yake makuu nchini Bolivia kwenda Medellin kucheza mechi ya dhidi Atletico Nacional.


Taarifa zimeeleza, ndege hiyohiyo mara ya mwisho iliwabeba wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kwenda kuwavaa Brazil, pia ikawabeba wachezaji wa timu ya taifa ya Venezuela.

1 COMMENTS:

  1. Kwanin unasema wameuwawa na hujaandika kitu kuashiria wameuwawa?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV