December 5, 2016


Klabu ya Simba, imemalizana na kipa Daniel Agyei kutoka Medeama ya Ghana na sasa kipa huyo ni mali ya Msimbazi.

Agyei mmoja wa makipa mahiri nchini Ghana amesajili mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.


Kipa huyo amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye pia alisaini kwa niaba ya klabu hiyo.

Kipa huyo alikamilisha mazungumzo na Simba jana, leo wakakaa na kujadili masuala kadhaa huku yeye akiukagua mkataba wake kabla ya kumwaga wino na kesho, anatarajia kuanza mazoezi rasmi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic