December 5, 2016


Bilionea Mohammed Dewji ameamua kuachana na kuendelea kuisaidia klabu ya Simba kwa madai mchakato ulioanzishwa na Hamisi Kilomoni kuzuia mkutano ulioitishwa, kulenga kuanzisha migogoro na mwisho kuondoa utulivu.

Taarifa zinasema Mo ambaye atoa zaidi ya Sh milioni 630 kwa miezi minne tu, ametoa masharti kwa kuwaeleza viongozi akiwa “mkavu” kabisa, hakuna mkutano wa mabadiliko, yeye anakitoa!

“Unajua mzee Kilomoni ameanzisha vurugu, anasema kwamba wanachama wamekwenda kwake kulalamika na hajawataja wangapi. Katuambia hakuna mkutano, yeye basi maana hataki malumbano tena. Anaomba mwisho inaweza kuwa aibu kwake.

 “Mo alikuwa akiisaidia Simba sana, ndani ya miezi minne katoa zaidi ya milioni mia sita thelathini,” kilieleza chanzo ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo

“Lengo lake lilikuwa ni kufikia mabadiliko na alijua katiba inafuatwa kwa kuwa wanachama wangekutana na kujadili. Kuzuia mkutano ni kuzuia kila kitu Simba.

“Kuna taarifa kwamba Kilomoni na Ramesh Patel hawataki mabadiliko, ni kama vile kina mzee Akilimali na Yanga. Hivyo wanachombeza chinichini, mbaya zaidi hawana hoja za msingi, ilimradi tu waivuruge Simba ikose ubingwa halafu waseme uongozi umefeli!”

Mchanganuo unaonyesha Mo aliwapa Simba Sh milioni 80 mara nne ikiwa ni mishahara ya miezi minne, alitoa Sh milioni 100 ambayo alikabidhiwa Rais Evans Aveva kwa ajili ya usajili.

Halafu wiki iliyopita akatoa tena Sh milioni 110 kusaidia usajili wa kipa Daniel Nana Agyei kutoka Ghana pia kuchangia kumbakiza Mohamed Hussein Zimbwe na wengine.

Kama haitoshi, Sh milioni mia ambazo amechangia katika masuala mbalimbali, Mo amekuwa akitoa Sh milioni tano katika kila mechi Simba iliyoshinda na katika mzunguko wa kwanza imeshinda mechi 11, sare mbili na kudungwa mbili.

Uamuzi wa Mo, utaipa Simba wakati mgumu kiuendeshaji katika duru la pili Ligi Kuu Bara na hasa katika suala la mishahara ikizingatiwa kwa sasa haina wadhamini.


Juhudi za kuwapata Kilomoni na Patel zinaendelea kwa kuwa wanaelezwa kuwa chanzo cha kuzuia mabadiliko yaliyomfanya bilionea huyo kuwa na hofu ya kuingia kwenye migogoro.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic