December 6, 2016

ISMAIL KHALFAN 'ISMA' WAKATI WA UHAI WAKE.


Sababu ya kifo cha mchezaji Ismail Alphan wa Mbao FC U20

Madaktari wa wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, wametoa ripoti ya kifo cha mchezaji wa Mbao FC, Ismail Khalfan.

Madaktari wamesema Ismail ambaye alianguka na kufa uwanjani, kifo chake kimetokana na kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA).

Ripoti hiyo imetolewa na Jeshi la Polisi Tanzania mkoa wa Kagera limethibitisha hilo.

Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini kusimama ghafla kwa moyo(sudden cardiac arrest) kulisababisha kifo. 

SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:

Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.

Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache mno.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic