December 13, 2016



Mashabiki wa Simba wameendelea kuonyesha ushirikiano na kikosi chao baada ya kumzawadia kiungo wao mshambuliaji, Shiza Kichuya.

Tuzo hiyo ilitolewa mara tu baada ya mechi ya kirafiki kati ya Simba iliyolala kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, jana.

Kundi la mashabiki wa Simba la mtandaoni maarufu kama Simba Sporaa likiongozwa na viongozi wake, Geff Kapyata Shimwela na Ally Masaninga pamoja na wanachama kadhaa wa kundi hilo, walikabidhi zawadi kwa Kichuya.

Kundi hilo limempa Kichuya zawdi ya mchezaji bora wa kundi hilo kwa mwezi Oktoba. 

Kundi hilo limetoa zawadi inayojumuisha Sh 500,000, viatu vya mpira na flemu yenye picha ya mchezaji huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic