December 5, 2016

MANDAWA

Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, imegomea kumtoa mshambuliaji wake tegemeo, Rashid Mandawa kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba, kutokana na kuwa na mipango naye katika kikosi hicho kufuatia kuhitaji kusuka upya kikosi chao ili kupata kina Shiza Kichuya wapya.

Mtibwa Sugar ndiyo timu ambayo inaongoza kwa kutoa wachezaji kwa timu mbalimbali kwenye ligi kuu kutokana na uwezo wake wa kuzalisha wachezaji kwenye timu.

Miongoni mwa wachezaji waliotoka Mtibwa Sugar na kufanikiwa kufanya vyema ni pamoja na Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Ame Ally, Hassan Kessy na wengineo ambao wate wanaonekana kufanya vyema.

Aidha, Mandawa ni miongoni mwa wachezaji kadhaa ambao walikuwa wakinyemelewa katika usajili wa dirisha dogo, hususani timu ya Simba ambayo ipo katika mkakati wa kusaka mshambuliaji mmoja wa ndani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amefunguka kuwa, kwa upande wao hawana mpango wa kumtoa mchezaji huyo katika timu yoyote kwa sasa kati ya Simba au timu nyingine itakayomhitaji, kwa kuwa wapo katika kipindi cha kujenga timu yao na kuhakikisha inakuwa katika ubora unaotakiwa ili kuleta ushindani kwenye ligi.

“Siwezi sema kama Simba walikuja ama hawajaja juu ya kumtaka Madawa, lakini kwa upande wetu, hadi sasa hatujaamua kumtoa mchezaji wetu yeyote katika timu yoyote katika usajili huu unaoendelea, kwani kwa sasa tunahitaji kujenga timu yetu.

“Tunahitaji kukitengeneza kikosi chetu kuhakikisha kinakuwa na ushindani wa hali ya juu, kwani kuna wachezaji wengi ambao tumewatoa kama kina Kichuya, Kessy, hivyo tunahitaji kukijenga kikosi chetu kwa kupandisha wachezaji wa kikosi cha pili na kuwachanganya na hawa tulionao ili kujenga timu imara,” alisema Kifaru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic