December 4, 2016


Mmoja wa wanachama maarufu zaidi wa klabu ya Yanga, Yusuf Mzimba (84) anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao Msoga mkoani Pwani.

Mwili wa Mzimba aliyefariki jana, unatarajia kusafirishwa leo kutoka jijini Dar es Salaam hadi Msiga.

Mzimba anakumbukwa kwa umahiri wake wa kuwapigania Wanayanga wa muda mrefu wakati wa kipindi cha mvutano mkubwa kati ya Yanga Kampuni na Yanga Asili aliyokuwa akioongoza.

Wanayanga mbalimbali wameendelea kumjadili huku wakizungumzia upambanaji wake wakati akiwa mwenyekiti wa Yanga Asili.

Mvutano huo uliochukua zaidi ya miaka minne, ulimalizwa na msuluhishi Yusuf Manji.

Manji alimaliza mgogoro huo baada ya vikao kwa takribani mwezi mzima mfululizo na mwisho wakaungana pamoja.


Upande wa Yanga Kampuni, ulikuwa unaongozwa na Abbas Tarimba aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, wakati huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic