Simba imechapwa kwa mabao 2-1 katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Kipigo cha Simba, kinapunguza makali ya watani wake Yanga ambao walichapwa kwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar.
Kipigo cha Yanga kiliwaamsha Simba ambao walitumia muda mwingi kuwananga watani wao, lakini leo mambo yamegeuka. Unaweza kusema hakuna kuchekana kwa kuwa Yanga ndiyo wanaotamba sasa.











0 COMMENTS:
Post a Comment