December 6, 2016




Beki Vincent Bossou amerejea mazoezini Yanga na kuanza mazoezi kwa kasi.

Beki huyo raia wa Togo, ameonekana akifanya mazoezi chini ya benchi jipya la ufundi chini ya Kocha George Lwandamina.

Lwandamina amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm ambaye aliinoa Yanga kwa misimu miwili mfululizo.

Bossou alikuwa akihusishwa kutaka kuhamia Vietnam lakini mambo yakaenda mlama.

Lakini yeye, juzi kupitia mitandao ya kijamii alilalamika kupotoshwa kwa habari zake kuhusiana na suala hilo la Vietnam, kwamba haikuwa sawa hata kidogo.

Awali, aliliambia gazeti la Championi alikwenda huko kumsimamia mdogo wake katika masuala ya mkataba.

Lakini Gazeti la Mwanaspoti liliripoti kwamba alizuiwa uwanja wa ndege kwa kuwa alikuwa anakwenda kufanya majaribio na hakuwa na barua kutoka Yanga inayoruhusu afanye majaribio nchini humo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic