December 5, 2016



Kinda wa Mbao FC ya Mwanza, Mrisho Khalfan amefariki dunia leo baada ya kuanguka uwanjani alipogongana na beki wa Mwadui FC katika michuano ya Ligi ya Vijana U20 inayoendelea.

Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na juhudi kubwa zilifanyika kuokoa maisha ya kinda huyo, lakini haikuwezekana.

“Inaonekana alishafariki dunia pale uwanjani, tulifanya juhudi kubwa mimi na wenzangu. Tulisaidiana na watu wengine pia waliokuwa uwanjani, lakini ilionekana hakukuwa na majibu mazuri,” alisema mmoja wa madaktari waliojaribu kuokoa maisha ya kijana huyo.

Mwenyezi Mungu Amrehemu.













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic