December 8, 2016





Wanachama kadhaa wa Simba, wametinga mahakamani na kuweka pingamizi la mkutano wa Simba uliopangwa kufanyika Jumapili.

Mkutano wa Simba, uliitishwa na uongozi wa klabu ikiwa ni kujadili masuala kadhaa likiwemo suala la mabadiliko.

Tayari mfanyabiashara bilionea, Mohammed Dewji maarufu kama Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 na kuwekeza Simba.

Lakini kuna wanachama wa Simba wamekuwa wakipinga hilo ingawa idadi yao inaonekana ni ndogo sana.


Wanachama hao wamewasilisha pingamizi hilo katika mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic