December 8, 2016


Kiungo James Kotei ameenda mjini Morogoro ambako ataungana na wachezaji wengine wa Simba.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema wanatafuta kiungo mkabaji kuziba pengo la nahodha Jonas Mkude ambaye amekuwa akiwadengulia hasa lilipofikia suala la usajili.

Simba imeweka kambi mjini Morogoro na Kotei raia wa Ghana alitua nchini jana, leo amekwenda kujiunga na wenzake.

Taarifa za awali za Simba zilieleza mchezaji huyo Mghana anakuja nchini kufanya majaribio.

Lakini taarifa nyingine ilizozipata SALEHJEMBE zimeeleza, Kotei atasaini mkataba wa muda mfupi na inawezekana kuwa ni miezi sita ili Simba ijiridhishe.


Kabla ya kuja nchini juzi, kiungo huyo aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Oman ambako inaelezwa hakupata nafasi ya kutosha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic