December 2, 2016



Klabu ya Yanga na Serikali wameingia mkataba kwa ajili ya klabu hiyo kuutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na ule wa Uhuru kwa ajili ya michezo yao ya Ligi Kuu Bara na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mkataba huo kati ya serikali umesainiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit aliyeiwakilisha klabu hiyo kongwe zaidi nchini.

Yanga imeruhusiwa kuvitumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani lakini imetakiwa kuvitunza wakati wa matumizi.

Utunzaji huo, unahusisha mali pamoja na vifaa vyote ndani ya viwanja hivyo.

Iwapo kutatokea tatizo na hasa uharibifu, basi Yanga ndiyo wakaohusika na matengenezo kwa gharama yoyote.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic