January 30, 2017



Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema hivi sasa kila mchezo kwao ni fainali.

Akizungumza Niyonzima amesema wamejipanga kuona wanafanikiwa kushinda kila mechi bila ya kujali ni timu gani wanakutana nayo kwani wanahitaji kupata pointi tatu katika kila mchezo.

“Mzunguko wa pili ni mgumu kila mechi unayokutana nayo inakuwa na ushindani, hivyo tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kuibuka na pointi tatu katika kila mchezo ili tuweze kufanikiwa kutetea ubingwa wetu, hakuna timu tunayoihofia, kila mechi kwetu ni fainali.

“Tunahitaji kufanya vyema kimataifa, hivyo lazima tuongeze juhudi kwenye ligi ili kuendelea kujiweka vizuri zaidi kabla hatujaanza mbio za kimataifa,” alisema Niyonzima.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV