January 30, 2017Baada ya kuitungua Simba, mshambuliaji na nahodha wa Azam, John Bocco, ametangaza kuwa kila mchezo wao ni fainali ambapo wataendelea kugawa dozi hata wakikutana na Yanga.

Bocco aliibuka shujaa kwa upande wa timu yake baada ya kuifungia bao pekee katika mchezo dhidi ya Simba uliomalizika kwa Azam kushinda bao 1-0. Mechi ilipigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Nahodha huyo amesema kuwa, baada ya kumaliza mchezo huo akili zao wanazipeleka katika michezo ijayo kuhakikisha wanafanya vizuri ili kumaliza kwenye nafasi nzuri.

“Tulishindwa kuwafunga Simba kipindi cha kwanza kwa sababu hatukuweza kuwasoma vizuri wapinzani wetu ila kipindi cha pili ilikuwa rahisi baada ya kocha kuwasoma na kutupa mbinu ambazo ndizo zimechangia kupata matokeo haya.

“Sasa kila mechi kwetu ni fainali na tutapambana ili tupate ushindi hata kama wakija Yanga nao ni lazima wapate kipigo kwani tumedhamiria kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobakia,” alisema Bocco.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV