January 12, 2017


Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam na kupewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea mazoezini.

Yanga ilirejea jijini Dar es Salaam jana, wachezaji wakaanza mapumziko jana na leo na kesho watarejea mazoezini kuendelea na maandalizi.

Yanga wameshindwa kuvuka katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi baadaya kutolewa na watani wao Simba.

Yanga imefungwa kwa jumla ya mikwaju ya penalti 4-2 baada ya mechi kwisha kwa dakika 90 bila ya bao.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wako katika nafasi ya pili nyuma ya watani wao, Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV