January 3, 2017


Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kikosi chao kina mipango yake na hakiwezi kucheza kwa presha ya kuangalia Yanga imefanya nini.

Mgosi amesema hayo kutokana na ile hali ya kuonyesha baadhi ya mashabiki hawafurahishwi na ushindi kiduchu kama ule wa mabao 2-1 dhidi ya Taifa Jang’ombe huku watani wao Yanga wakiwabutua Jamhuri kwa mabao 6-0.

Mgosi ameiambia SALEHJEMBE kwamba, Simba ni timu yenye mipango yake na si fuata mkumbo kwa kila jambo.

“TUnataka kushinda na ikiwezekana ni mabao mengi. Inapotokea kuna makosa au mazuri basi kocha anayafanyia kazi.

“Ushauri wangu tumuache kocha afanye kazi, kitu kizuri Simba imeshinda na kupata pointi tatu. Tusiwape wachezaji presha za bila sababu, si lazima tushinde kama Yanga.

“Kuna wakati tunaweza kufanya hivyo au tusifanye. Huu ni mpira jamani, tuwe waelewa. Mashabiki watuunge mkono na sisi tunajitahidi sana kutowaangusha,” alisema Mgosi aliyekuwa mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo kabla ya kustaafu.

Mashabiki wa Simba, hasa kupitia mitandao mbalimbali wamekuwa wakilalamika kutokana ushindi wanaoona ni mwembamba.


Ikionekana wazi hali hiyo inatokana na Yanga kuivurumisha Jamhuri kwa rundo hilo la mabao sita, jambo ambalo wangependa kuona linatokea kwao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic