January 28, 2017
Daktari wa Muhimbili amewaambia Simba waondoe hofu, wanaweza kumtumia Abdi Banda katika mechi dhidi ya Azam FC leo.

Simba inaivaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Jana, Simba walikuwa na hofu  baada ya Banda kuumia nyama za paja na akalazimika kwenda kufanyiwa vipimo.

“Jana jioni sana, daktari kasema Banda anaweza kucheza, hakuumia sana,” kimeeleza chanzo cha uhakika.

Jana asubuhi, Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi alisema Banda asingecheza mechi ya leo.


“Matumaini ya kucheza ni kama asilimia ishiriki au thelathini kwa mujibu wa dokta. Lakini atakwenda kufanyiwa vipimo,” alisema Mgosi hiyo jana.

Banda amekuwa tegemeo la safu ya ulinzi ya Simba hasa baada ya kuondoka Juuko Murshid. Amekuwa akishirikiana vizuri na mkongwe Method Mwanjale na kuendelea kuifanya Simba kuwa na safu imara zaidi ya ulinzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV