January 28, 2017




Nahodha wa Azam FC, John Bocco, amemfunika Emmanuel Okwi kwa ufungaji katika mechi za Ligi Kuu Bara zilizozikutanisha Simba na Azam tangu mwaka 2011.


Katika mechi 17 za ligi hiyo kati ya Azam na Simba, Bocco amefunga mabao sita huku Okwi ambaye sasa hana timu akiwa amefunga matano tu.


Rekodi hiyo ya Bocco inaweza kuendelea leo  kwani mchezaji huyo anaweza kuichezea Azam dhidi ya Simba katika muendelezo wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Bocco alianza kuifunga Simba katika mchezo uliochezwa Januari 23, 2011, ambapo aliifungia Azam mabao mawili na kuiwezesha kushinda kwa mabao 3-2.


Straika huyo alifunga bao la tatu katika msimu wa 2012/13, Oktoba 27, 2012 ambapo licha ya kufunga bao moja, Azam ilifungwa mabao 3-1 na Simba. Machi 29, 2014, Bocco aliifunga Simba bao la nne ikiwa ni katika msimu wa 2013/14.

Desemba 12, 2015 katika sare ya mabao 2-2, Bocco alifunga mabao mawili ikiwa ni katika msimu wa 2015/16. Okwi aliyevunja mkataba na Klabu ya Sonderjyske ya Denmark, aliifunga Azam bao la kwanza Februari 11, 2012 katika msimu wa 2011/12, ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.


Oktoba 27, 2012, Okwi alifunga mabao mawili kwenye mechi moja ambapo Simba iliifunga Azam mabao 3-1, hiyo ilikuwa msimu wa 2012/13.



Okwi alifunga bao lake la tano Januari 25, 2015,  katika msimu wa 2014/15, ambapo Simba na Azam zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mchezo huo, Okwi aliumizwa na beki wa Azam, Aggrey Morris na kupoteza fahamu kisha akakimbizwa hospitalini.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Nafikiri si sahihi kumlinganisha mchezaji aliyecheza club tofauti tofauti na Boko aliyecheza timu moja tu,Okwi kwa nyakati tofauti amezichezea Simba,Young,Simba na akaenda ulaya,sasa unamlinganishaje na Boko ambaye siku zote yupo Azam akiendelea kushiriki michezo yote dhidi ya Simba?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic