January 28, 2017



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi wake kuhusiana na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kumteua mwamuzi Martin Saanya kuchezesha mechi za kimataifa wakati amefungiwa na TFF kujihusisha na soka.


Hivi karibuni Caf ilimtangaza Saanya kuwa mmoja kati ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika namba 18 utakaozikutanisha Vital’O ya Burundi na Mountana ya Sudan.


Akizungumza Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema: “Saanya ni mwamuzi wa Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa), hivyo kitendo cha kufungiwa kuchezesha mechi za Ligi Kuu Bara hakiwezi kumzuia kuchezesha mechi za kimataifa ambazo zinasimamiwa wa Caf pamoja na Fifa.


“Baada ya kuvurunda katika mechi za ligi kuu tulizompatia achezeshe, tukaona hatufai, hivyo tukaamua kumweka pembeni lakini Caf wao wameona anafaa kwa sababu alifanya mtihani wao pamoja na ule wa Fifa akafanya vizuri, hivyo wana haki ya kumtumia.”


TFF ilimfungia Saanya pamoja na aliyekuwa msaidizi wake katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Samuel Mpenzu katika mchezo uliozikutanisha Simba na Yanga Oktoba Mosi, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kuvurunda mechi hiyo kwa kutoa maamuzi yenye utata likiwemo tukio la kumwonyesha kadi nyekundu Jonas Mkude wa Simba.


Pia Saanya alishindwa kutoa maamuzi sahihi juu ya bao la Yanga ambalo lilifungwa na Amissi Tambwe ambaye kabla ya kufunga alidaiwa kuushika mpira.


1 COMMENTS:

  1. Kutumia kwa mo ni pengo kubwa sana kwa simba hasa ukizingatia washambuliaji wote sasa wako butu..na tegemeo la simba sasa limebaki kwa mo na mzamiru ambao wanaoweza kupiga mashuti ya kulenga lango..simba sasa tunaweza kulinda na kucheza katikati lakini hilo halitoshi kama hatutafunga mwisho wa siku tukifungwa haturudishi..na hili nafikiri ni kwa sababu ya mfumo anaoutumia kocha wa washambuliaji kurudi nyuma sana kuja kukaba staili ya kupaki basi na mbele panakuwa hakuna mtu anayekuwa tayari kupokea mipira na kutumbukiza nyavuni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic