January 11, 2017Kocha wa zamani wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuinoa timu ya Asante Kotoko ya Ghana baada ya kuachana na Interclube ya Angola.

Logarusic ambaye aliinoa Simba kuanzia Desemba, 2013 mpaka Julai, 2014, Novemba mwaka jana alimaliza mkataba wa kuifundisha Interclube huku akifanikiwa kuipa kombe la chama cha soka la nchi hiyo, APFL.

Mtandao wa habari za michezo wa Ghana unaojulikana kama Ghana Soccernet, jana Jumanne uliripoti kuwa: 

“Asante Kotoko imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha raia wa Croatia, Zdravko Lugarusic, ataanza kuinoa timu hiyo ndani ya wiki hii baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali cha kazi.”

Ikumbukwe kuwa, Asante Kotoko ilikuwa haina kocha mkuu tangu Machi, mwaka jana baada ya aliyekuwa kocha wao, David Duncan kuachia ngazi kutokana na matokeo mabaya aliyokuwa akiyapata. Kwa muda wote huo, kikosi hicho kilikuwa chini ya kocha msaidizi, Michael Osei.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV