February 13, 2017


Kocha wa Man City, Pep Guardiola anaonekana yuko kwenye wakati mgumu kutaka kupata kombinesheni ya uhakika katika ushambulizi.

Anataka washambulizi watatu hatari wanaoelewana kama ilivyo kwa Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez wanaounda MSN katika kikosi cha Barcelona.

Tayari ameanza kuwatengeneza vijana Rahim Sterling, Gabriel Jesus na Leroy Sane ambao kama watafanya anavyotaka, huenda akawa na uhakika na kupunguza presha.


Bado mambo hayajakaa kama anavyotaka na Ligi Kuu England imeonekana ni si laini kwake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV