February 12, 2017


Mshambuliaji gwiji wa Arsenal, Thierry Henry amesema kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante anastahili kushinda tuzo maarufu ya Ligi Kuu England ya PFA.

Tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa msimu England, ndiyo kubwa zaidi nchini humo kwa wachezaji.

Henry amesema Kante ambaye anatokea Ufaransa kama yeye, anastahili kushinda tuzo hiyo akitumia kigezo cha alivyoisaidia Leicester City kubeba ubingwa msimu uliopita.


Lakini akaongeza mwendo wa Chelsea sasa na inaelekea kubeba ubingwa, Kante akiwa ndiyo injini ya timu.


Henry ni kati ya wachezaji waliowahi kubeba tuzo hiyo wakati akikipiga Arsenal kwa mafanikio makubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV