February 8, 2017
Kocha wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kwa sasa kikosini kwake hakimtegemei mchezaji mmoja kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo unaofanana.

Cheche ameyasema hayo baada ya kuwakosa nyota wake wanne kwenye mechi mbili walizocheza ambazo waliweza kukusanya pointi nne kati ya sita.

Wachezaji hao aliowakosa ni John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Stephane Kingue na Shomari Kapombe ambao wanasumbuliwa na majeraha mbalimbali.

Hawa walishindwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelod Sundowns waliyotoka suluhu na mchezo wa Ligi Kuu Bara walioibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda.
Akizungumza na Championi Jumatano, Cheche alisema:

 “Hapa hatumtegemei mchezaji mmoja, kama huyu akikosekana basi yupo mwingine ambaye naye anaweza kuziba pengo kiufasaha zaidi.“Mechi mbili tumecheza bila ya wachezaji wetu wanne ambao ni wa kikosi cha kwanza, lakini matokeo tuliyoyapata si mabaya, tumeshinda na sare, hivyo sina wasiwasi ikitokea wachezaji wangu wa kikosi cha kwanza wamepata majeraha, wapo watakaokuja kucheza nafasi zao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV