February 17, 2017



Maandalizi ya mchezo wa kesho wa kimataifa kati ya Young Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, yamekamilika kwa asilimia 100.


Timu zote zipo Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi, Dar es Salaam.


Kwa upande wa timu ya N’gaya, yenyewe imefikia Hoteli ya Kaluganje iliyoko Mtaa wa Gerezani, Kariakoo wakati waamuzi kutoka Uganda, pamoja na Kamishna wa mchezo wanatarajiwa kutua leo.


Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda ambano ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.


Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic