February 17, 2017




NA HAJI S MANARA

Afe kipa afe beki, kufungwa watafungwa tu.

Nn Haji anajivunia kuelekea feb 25?

Mpira ni mchezo unaochezwa hadharani, hauchezewi chumbani, na mpira ni mchezo wa takwimu, hasa huu mpira wa kisasa, kuelekea feb 25 Simba anaongoza ligi na ameongoza kwa raundi nyingi ni zaid ya 90%ya mizunguko yote tuliocheza hadi sasa

Achana na kuongoza ligi ,Simba ndio timu pekee hadi sasa iliyofuzu kwa robo fainali ya kombe la Shirikisho,wengine watafata tu.

Takwimu pia znatubeba,tumeongoza kwa kumiliki mpira ktk michezo yote ya ligi kuu na kombe la shirikisho, kuliko timu yoyote hadi sasa, hata kwenye michezo iliyopoteza, Simba walikuwa bora ktk umiliki wa mpira uwanjani, mbali ya team iliyotengeneza nafasi nyingi za magoli kuliko timu yoyote ya ligi kuu msimu huu.

Ukiachana na hilo nani anabisha Simba ndio timu yenye ukuta mgumu ktk ligi kuu? tukiruhusu wavu wetu kutikiswa mara saba tu? sijui kama wajua pia, Simba haijawah kufungwa mchezo wowote ule kwa tofauti ya goli moja, wenzetu hadi NNE washachezea!!

 Najua wafahamu pia kwa sasa hakuna beki imara anayemfikia walau nusu Method Mwanjale!!sijui nn niseme kuhusu Ajibu,Mavugo na MO!!

wakitoka wakapige mnada lile jengo lao liliokuwa bondeni kule wanapofugia chura.

Hz ni takwimu na namba, wazungu wanasema numbers dont lie, namba haziongopi, tutawafunga, narudia tutawafunga,TUTAWAFUNGA bila wasiwasi.

Uzuri wake tupo vzuri ndani na nje ya uwanja,hatuna makando yoyote hata ktk uongozi,tumetulia tuliii kama barafu,wenzetu ndio hvyo tena kama mlivyosikia!!

Kikubwa waamuzi waje kuchezesha kwa kufuata sheria 17, TFF wanajua na nchi inajua, tunataka mshindi halali, hatutaki kubebwa na hatutakubali kuonewa, huku pia tukiwataka washabiki wetu wawe watulivu,na tunaenda kujaza uwanja, kila mwana Simba na aje, avae jezi zetu na tununue mapema tiketi zetu kupitia Selcom.

Twendeni tukawadhalishe Taifa feb 25, twendeni mkamuone king Loudie, twendeni mkauone udambwi wa MO na Ajibu, twendeni mkazione Sambusa za mboga mboga pale Taifa, tutahanikiza mwanzo mwisho huku tukiwacharura wenzetu kwa mambo yao yaleeeeee...

Ahhh ntaandika daily kuelekea feb 25, leo mwanzo tu.


Ijumaa njema

6 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. mjiandae kupunguza magoli tu maana hakuna namna kwa fowadi hii ngoma,tambwe,chilwa na msuva sijui yangu macho tu

    ReplyDelete
  3. Wekundu wa msimbazi kwa sasa hawakamatiki,changanya na dozi waliyoenda kuchukua unguja,yebo lazima achezee 4G

    ReplyDelete
  4. sawa manara,nakumbuka nilisema huu ndio muda wako wa kuongea, lakini 25/2 sio mbali, utaprove maneno yako saa 1 jioni ya siku hiyo. unawaona yanga ni uji sana hadi umfananishe mwanjale na bossou siyo, msuva na Mo, ajibu na Ngoma etii?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic