February 12, 2017
Kocha George Lwandamina amesema wako vizuri na wanajiandaa kufanya vema katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ngaya ya Comoro, leo.


Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Moron, Comoro, Lwandamina amesema hakuna wanachoweza kulaumu.


“Hadi sasa kila kitu kinakwenda vizuri na tunamshukuru Mungu tulitua salama.


“Hakuna tunachoweza kulalamika, mambo yanakwenda vizuri na tutaendelea na maandalizi ya mwisho,” alisema.Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kuwavaa wenyeji wake katika mechi ambayo inaonekana haitakuwa rahisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV