February 1, 2017


Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza hali ya kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny si nzuri na amelazwa.

Taarifa hizo zinaeleza Bonny maarufu kama Ndanje amelezwa katika Hospitali ya Makandana huko Tukuyu mkoani Mbeya.

Taarifa zinasema hali yake si nzuri na alikuwa ametundikiwa diripu ingawa hatujajua hasa kinachomsibu.


Kama wewe ni mwamanichezo na unaona uko karibu na maeneo hayo na unaweza kuwa sehemu ya msaada kwa Bonny ambaye pia aliwahi kuitumikia Tukuyu Stars na timu ya taifa, Taifa Stars. Tafadhari fika na kuongeza nguvu ya kumsaidia mchezaji huyo ambaye ni mmoja wa wanamichezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV