March 20, 2017Mshambuliaji Frederic Blagnon amesema amefurahishwa kufunga bao akiwa ndiyo amerejea Simba.

Blagnon amefunga bao wakati Simba ikiishinda Mererani FC bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa mjini Mererani mkoani Arusha.

“Nimefurahi sana, najua Mererani si timu kubwa lakini ilionyesha soka safi. Najua kufunga kunanipa morali ya kurejea vizuri, nataka kufunga zaidi ikiwezekana,” alisema.

Blagnon alisema kama hatafunga, basi angependa kuwa msaada katika timu ili kuhakikisha wanaikamilisha vizuri safari yao ya kutwaa ubingwa.

Blagnon ambaye alijiunga na Simba akitokea nchini Ivory Coast alishindwa kuonyesha cheche hadi uongozi wa Simba ulipoamua kumpeleka Oman kwa mkopo, hata hivyo amerejea kutokana na kibali chake kuchelewa kutumwa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV