April 24, 2017



Barcelona imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi yao ya El Clasico wakiifunga Madrid kwa mabao 3-2.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Bernabeu mini Madrid, wachezaji wa Barcelona walikimbia kilomita 7 zaidi ya wale wa Madrid.

Ingawa Madrid walicheza pungufu mtu mmoja katika dakika 13 za mwisho lakini takwimu za La Liga zinaonyesha wachezaji sita wa Barcelona walikimbia zaidi ya kilomita 10.

Kiungo Sergi Roberto aliyewachachafya Madrid katika dakika ya mwisho na kutoa pasi murua kwa Messi aliyemaliza kazi, alikimbia zaidi ya kilomita 12.

Beki wa pembeni Jordi Alba, viungo Sergio Busquets, Gerard Pique na mkongwe Andres Iniesta walikimbia kilomita 11.

Kipimo cha ubora kinaonyesha wamekimbia zaidi ya walivyokuwa wakifanya katika mechi za nyuma, hali inayoonyesha kweli walicheza kwa juhudi kubwa mechi hiyo.

Kwa wa Madrid, wengi hawakuwa katika kiwango cha juu na inaonekana wachezaji wawili tu. Beki wa kulia Dani Carvajal na kiungo Mjerumani, Toni Kroos ndiyo walikimbia zaidi ya kilimita 10.

Kama utajumlisha, unapata Madrid wakiwa katika kiwango cha chini katika ukimbiaji.


Kwa ujumla Barcelona walikimbia 105.46km, wakati Madrid wanaonolewa na Zinedine Zidane walikimbia 98.75km.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic