April 24, 2017
Uongozi wa Klabu ya Yanga umewataka wanachama na wapenzi wa timu hiyo kongwe hapa nchini kuichangia kwa hali na mali katika kipindi hiki ambacho wamekumbwa na matatizo ya kifedha tangu Mwenyekiti wake, Yusuf Manji apate matatizo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa leo Jumatatu baada ya uongozi wa timu hiyo kuingia makubaliano na Kampuni ya Selcom kwa ajili ya kuendesha zoezi maalum kwa ajili ya wanachama wa timu hiyo kuweza kuichangia timu yao.

“Tumeingia makubaliano na Selcom kwa miezi mitatu ya kutuendeshea zoezi la wanachama wetu kutuchangia fedha kwenye kipindi hiki ambacho tumekuwa na matatizo kidogo juu ya fedha am,bapo makubaliano hayo yataendelea zaidi baada ya kuona faida ambayo tutaipata katika wakati huo.

“Wanachama watachangia klabu kwa njia ya mitandao ya simu kupitia huduma za kutuma fedha kwa njia ya kimtandao, ambapo kwa sasa tunawaomba wanachama na mashabiki wote kuichangia timu kwa vile wanavyoweza,”alisema Mkwasa.


Mkwasa aliitaja namba ya kuchangia ni 150334 ambayo watumiaji wa mitandao yote ya simu za mkononi wanaweza kuitumia kuchangia klabu yao.
 

1 COMMENTS:

  1. Viongozi wa hizi timu za Simba na Yanga lini jamani mtaacha ombaomba mnatia aibu hizi Club,wekeni mipango ya kudumu hizi timu zijiendeshe,wanachama sio lolote zaidi ya makelele tu,Binaifisheni hizi timu,ni aibu tu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV