April 30, 2017



MPIRA UMEKWISHA
-Niyonzima anapoteza nafasi ya wazi kabisa hapa


DAKIKA 6 ZA NYONGEZA
Dk 89, Mbao FC wanaokoa mpira wa kona ya Niyonzima
Dk 87 krosi maridadi kabisa ya Niyonzima, Msuva anaruka peke yake, anapiga kichwa juuuu
Dk 86 sasa, Mbao FC wamerejea nyuma na wanaondosha kila mpira unaokuja huku wameacha mchezaji mmoja tu nyuma 
SUB Dk 83, Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 82 Tambwe anapoteza nafasi nzuri kabisa akiwa karibu kabisa na goli la Mbao FC
Dk 80 Cannavaro anapiga kichwa safi hapa lakini kipa Haule anaonyesha umahiri, anapangua na kuwa kona. Inachongwa na Mbao FC wanaokoa
Dk 77, Yanga wanapata kona tena, inachongwa kona fupi, Niyonzima anaachia shuti, Kipa Haule anaokoa na sasa yuko chini anagaagaa


Dk 76, mpira mwingine wa faulo, Juma Abdul anapiga lakini juuuuu
Dk 74, kipa wa Mbao anadaka mpira unamtoka na kuwa kona, inachongwa vizuri naye Benedict anadaka vizuri kabisa
Dk 73 Mpira wa adhabu wa Kamusoko, unatoka juu la goli la Mbao FC
SUB Dk 73 Ndaki Robert anaingia kuchukua nafasi ya Benard 
KADI Dk 70 Benard analambwa kadi ya njano kwa kupinga filimbi


Dk 68, Kamusoko anaachia mkwaju mkali wa adhabu lakini unapita juuu
SUB Dk 67, Yanga wanamtoa Kessy na nafasi yake inachukuliwa na Juma Andul Mnyamani
Dk 65, Yanga wanashambulia, shuti kali la Kamusoko linawababatiza mabeki wa Mbao FC ambao wanaokoa huku wachezaji wa Yanga wakilalama kwamba kuna beki wa Mbao alishika
DK 63 Pasi ya kichwa ya Tambwe, Niyonzima anaachia mkwaju hapa, nje.


Dk 61 Kamusoko anaingiza mpira wa juu hapa lakini Msuva anashindwa kuuwahi na kipa wa Mbao anapangua vizuri
Dk 61 Mwashiuya anaachia shuti kali hapa, linagonga mwamba na kutoka nje
SUB Dk 58, Habib Haji anaingia upande wa Mbao kuchukua nafasi ya Benard
KADI Dk 57 Jamal MWambeleko wa Mbao FC analambwa kadi ya njano kutokana na kumbishia mwamuzi 



Dk 52 sasa, Niyonzima yuko chini akitibiwa baada ya kuumizwa na wacheaji wa Yanga wanamlaumu mwamuzi kuwa hajatoa kadi
Dk 48 MSuva anaachia mkwaju mkali kabisa, Mbao wanaokoa na kuwa kona
SUB Dk 45, Goefrey Mwashiuya ameingia kuchukua nafasi ya Said Juma Makapu
Dk 45, Yanga wanaanza kwa kazi kubwa wakionekana wamepania kusawazisha

MAPUMZIKODAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Niyonzima anageuka na kuachia shuti kali sana lakini linapita juu kidogo ya goli la Mbao
Dk 42, krosi maridadi ya Kessy, lakini Tambwe anapiga na kutoa nje, goal kick


Dk 39 sasa, hakuna shambulizi jingine na zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja pekee
Dk 34, MSuva anaachia shuti kali lakini anapaisha juuuu
Dk 32 Mbao FC wanaonekana tena kurejea na kumiliki zaidi mpira katikati ya uwanja
Dk 29, Chirwa anainga vizuri lakini Maganga yuko makini, anaondosha
GOOOOOOOO Dk 27, krosi safi kutoka magharibi mwa uwanja uwanja, Vicent Andrew Dante anajifunga
Dk 23 Kamusoko anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, lakini kipa wa Mbao FC yuko makini, anadaka
Dk 23 sasa, Mbao FC ndiyo wanaonekana kuutawala mchezo kwa kiasi kikubwa huku Yanga wakilazimika kuokoa muda wote
Dk 18, shuti kali la Maganga lakini mpira unapita juu ya lango


Dk 14 sasa, bado mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makubwa Dk 8, Mbao FC wanapata kona hapa, inachongwa, Kessy anaokoa na kuwa kona nyingine...inachongwa goal kick
Dk 6, Yanga wanapata kona ya kwanza hapa, inachongwa hapa lakini goal kick
Dk 4 mpira safi wa krosi Chirwa anaukosa na kuanguka. Yuko chini hadi sasa
Dk 1, mechi imeanza kwa kasi na Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic