April 29, 2017




MPIRA UMEKWISHAAA
-Dakika 90+5 zimekamilika, lakini Agyei ndiyo anajivuta baada ya kupatiwa matibabu ili mechi iendelee
-Kapombe yeye na kipa Agyei, anashindwa kuuwahi mpira, wanagongana. Agyei yuko chini pale na madaktari wa Azam FC ndiyo wamewahi kuingia kumtibu kipa wa Simba ili mechi iendelee
-Bocco anaanguka hapa akiwania mpira na Boukungu lakini Mwamuyzi anasema cheza mpira
-krosi nzuri ya Blagnon lakini Ndemla anashindwa kuitumia
-SUB-anaingia Frederic Blagnon kuchukua nafasi ya Ajibu

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
SUB Dk 88, Ndemla anaingia kuchukua nafasi ya Kotei ambaye ameumia
SUB Dk 86 anatoka Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto
Dk 85, Kotei yuko chini pale baada ya kukaa tena, wanaingia kumtoa, inaonekana hataendelea
Dk 84 Agyei anakwenda Markiti, Bocco anapiga kichwa kinaenda wavuni lakini kabla ya kuvuka msitari, Bokungu anaondosha
Dk 82, Mavugo anaingia vizuri na kuachia shuti kali, linazuiwa na kuwa kona
SUB Dk 82 Mudathir Yahaya anaingia kuchukua nafasi ya Singano
Dk 80 sasa, Kotei yuko chini pale. Amelala, awali aliumizwa na Mahundi, akajitahidi akainuka. Baada ya dakika moja akarejea chini na kukaa
KADI NYEKUNDU Dk 77, Mo Ibrahim analambwa kadi ya pili ya njano alipomkanyaga Kampombe ambayo imezaa kadi nyekundu
Dk 75, Bocco anaachia mkwaju mkali wa adhabu, unamtoka Agyei halafu anadaka tena
Dk 72 Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya Mavugo kuikosa krosi safi ya Ajibu


Dk 68, Himid anaachia mkwaju mkali wa mpira wa Adhabu, Kichuya anaweka kichwa na unaokolewa
Dk 66, Manula anaonyesha umahiri akipangua shuti kali la Ajibu, sentimeta chache kutoka katika lango lake, inakuwa kona ya tano ya Simba, inachongwa na kuokolewa
Dk 65 sasa, mpira kama umepoa hivi, Azam FC wanaonekana kuwa makini zaidi katika ulinzi
Dk 61, Mo Ibra anatoa pasi nzuri kwa Mavugo, anaachia shuti kali, mpira unatoka sentimeta chache kidogo nje ya lango la Azam FC...ilikuwa hatari
Dk 61 Kichuya nje ya 18 anaachia shuti lakini linatoka nje
Dk 60 sasa, Simba wanaanza kuonekana kama wamepoteza ile hali ya umakini na kucheza kitimu


SUB Dk 58 anaingia Joseph Mahundi kichukua nafasi ya Kingue, sasa Azam FC wanataka kufunga na huenda wakatumia mipira ya mashuti kupitia kiungu huyu aliyeingia
Dk 56, Simba wanapata kona yao ya nne, inachongwa vizuri lakini wmisho Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 55 Muzamiru anaachia shuti kali, mpira unaguswa na kuwa kona, inachongwa, mpira unamfikia Mo Ibra tena, anaachia mkwaju mwingine lakini goal kick
Dk 53 krosi nyingine nzuri ya Bukungu, lakini Mavugo na Manula wanavaana na mwamuzi anasema offside
Dk 52 krosi nzuri inamfikia Mavugo, anashindwa kufunga, unakwenda kwake Kichuya naye anashindwa kufunga na Manula anadaka vizuri

Dk 51, mpira mzuri wa adhabu, anaruka juu Aggrey na kupiga kichwa vizuri, mpira unapita juu kidogo ya lango la Simba
Dk 50, Bocco anapokea pasi nzuri la Gadel, anaachia shuti lakini linakuwa kuuubwa
GOOOOOOOOOOO DK 48, krosi safi ya Mavugo, Mo Ibrahim anajipinda na kuachia mkwaju mkali unaomshinda Manula
Dk 47, Kapombe alitaka kufanya mzaha lakini Manula anaondosha mpira hup
SUB Dk 45 Shabani Iddi anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Frank Domayo, inaonekana Azam FC wameamua kupunguza mshambulizi, kuongeza kiungo kwa lengo la kusaidia kuzuia kuzidiwa katika kiungo. Domayo ni kiungo mlinzi, hivyo sasa Azam FC inacheza na viungo watatu wa ukabaji plus Stephan Kingue plus Himid Mao

MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
DK 44, Simba wanagongeana kwa dakika moja nzima bila Azam kuupata mpira lakini shuti Ajib linapaa juuu
Dk 42, Kichuya anapiga shuti tena lakini ni butu. Kila wanapoingia kwenye lango la Azam FC, Simba wanaonekana kutokuwa na utulivu
Dk 41, Kichuya anajaribu nje ya 18, lakini Manula anaonyesha utulivu kwa mara nyingine
Dk 39 Ajibu anaingia, anapiga krosi katikati ya lango la Azam chinichini lakini Manula anaifuata na kudaka vizuri


Dk 35, krosi nzuri ya Mo Ibrahim, Mavugo anaruka na kupiga kichwa lakini Manula anadaka vizuri na kuanguka chini hapa
Dk 34 krosi nzuri ya Gadiel Michael, Shabani anashindwa kufunga akiwa hatua moja na lango la Simba, anapiga kichwa kinakwenda nje
Dk 31, Mo Ibrahim anaingia vizuri lakini Manula anaonyesha umahiri na kudaka vizuri kabisa
Dk 30, Azam FC wamekuwa wakirudi nyuma wote na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza. Lakini Simba wanaendelea kusukuma mashambulizi mengi na kutawala katikati lakini si makali
KADI Dk 28, Bukungu analambwa kadi ya njano, inakuwa kadi ya tatu ya njano na moja nyekundu katika mchezo huu
Dk 25, krosi safi ya Zimbwe hapa, lakini Manula anapangua na Mao anaosha


Dk 25, Ajibu anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali hapa lakini umeguswa, kona
Dk 22 sasa, Azam F wanaendelea kusukuma mashambulizi na wanacheza vizuri kama hawako pungufu
Dk 19, Azam FC wanapata kona, inachongwa hapa Agyei anadaka, mpira unamtoka na Mkude anawahi na kuondosha
KADI NYEKUNDU....Dk 16, SUre Boy analambwa kadi nyekundu kwa kumuangusha tena Ajibu hapa
Dk 15, Ajib yuko chini hapa na analalama kwamba alipgwa kipepsi
Dk 14 sasa, timu zinacheza kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa uwanja unateleza sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha


Dk 10, Shabani anampiga chenga Agyei hapa, mpira unabaki kwa Singano yeye na lango hatua mbili tu mbele yake lakini naye anateleza na kuanguka chini
Dk 7, Mo Ibrahim anaingia krosi safi kabisa hapa lakini Mao anaokoa vizuri kabisa, ilikuwa hatari
KADI Dk 6 Mo Ibrahim analambwa kadi ya njano kutokana na kumfanyia madhambi Himid Mao
Dk 4, krosi nzuri kabisa ya Singano, hatari kabisa lakini anawahi Kotei
KADI  Dk 3, Aggrey Morris analambwa kadi ya njano kwa mchezo wa kindava
Dk 1, Simba ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Azam FC lakini Manula anadaka vizuri  

KIKOSI CHA SIMBA SC 
1-Daniel Agyei 
2-Javier Bukungu 
3-Mohamed Hussein 
4-James Kotei 
5-Juuko Murshid 
6-Jonas Mkude 
7-Shiza Kichuya 
8-Mzamiru Yassin 
9-Laudit Mavugo 
10-Ibrahim Ajibu 
11-Mohamed Ibrahim 

SUB 
-Peter Manyika Jr 
-Vicent Costa  
-Said Ndemla 
-Mwinyi Kazimito 
-Pastory Athanas 
-Juma Luizio 
-Fredrick Blagnon


KIKOSI CHA AZAM SC                         
1-Aishi Manula
2-Shomary Kapombe
3-Gadiel Michael
4-Daniel Amoah
5-Agrey Morris
6-Stephan Kingue Mpondo
7-Salum Abubakar
8-Himid Mao
9-John Bocco
10-Shabaan Iddi
11-Ramadhan Singano

SUB
-Mwadini Ally
-Erasto Nyoni
-Bruce Kangwa
-Yakubu Mohamed
-Mudathir Yahaya
-Frank Domayo

-Joseph Mahundi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic