April 30, 2017




RAUNDI YA 11:
Klitschko anaonekana kuzidiwa tokea mwanzo, Joshua anashambulia kama umeme, lakini Joshua anaonekana kama amchoka. Mwisho Klitschko anakosea, ngumi moja inaonekana kumlevya na Joshua anashambulia mfululizo na kumuangusha, Klitschko anahesabiwa na kurejea.

Joshua anamshambulia kama nyuki na kumuangusha, anainuka na kuendelea lakini anapigwa tena na mwamuzi anamuokoa Klitschko....JOSHUA AMESHINDA KWA TKO.


RAUNDI YA 10:
Klitschko anaonekana kufanya vizuri anamshambulia sana na mwishoni Joshua anaonekana kuchoka


RAUNDI YA 9:
Joshua anaonekana kubadili aina ya upiganaji kwa kupiga jab nyingi lakini Klitschko bado yuko imara. Joshua anaonekana kurejea vizuri



RAUNDI YA 8:
Joshua alianza vizuri na ndiye ameshambulia vizuri zaidi. Makonde mengi yanamfikia Klitshchko lakini mkongwe anapiga jab nyingi zaidi ambazo Joshua anapaswa kuwa makini

RAUNDI YA 7:
Hii raundi inaonekana haina mwenyewe kwa kuwa kila mmoja anajaribu kushambulia lakini raundi ya 5 na 6 inaonekana kuwachosha, hawakuwa na makeke sana.

RAUNDI YA 6:
Konde kali la mkono wa kulia, Joshua anakwenda chini, Klitschko ndiye anashambulia zaidi katika raundi hii, mara kadhaa Joshua analazimika kukimbia

RAUNDI YA 5:
Joshua anaonekana kuanza vizuri raundi hii akishambulia lakini mwishoni mpinzani wake naye anajitahidi kutulia baada ya kuhesabiwa na mwamuzi kutokana na kuwa na hali mbaya.

RAUNDI YA 4:
Klitshcko kaanza na kasi ya kimondo na ngumi zake tatu zinatua usoni kwa Joshua ambaye alikuwa hajajipanga, lakini baadaye akatulia na kujibu mashambulizi vikali hali iliyomlazimu Klitshcko kuanza kukumbatia. Mwisho Joshua ndiye amefanya vizuri zaidi

RAUNDI YA 3:
Joshua kaana raundi hii kwa kasi kubwa na kushambulia kwa ngumi za mfululizo. Hali ambayo ilionekana kumchanganya Klitchko ambaye baadaye aliweza kutulia na kuanza kujibu mashambulizi lakini hayakuwa makali kama ya Joshua

RAUNDI YA 2:
Joshua alianza kwa kasi, akatawala na kupiga kama ngumi tano nzuri, Klitshcko akajibu kama tatu na mwisho hakukuwa na mashambulizi zaidi ya kuvisiana tu


RAUNDI YA 1:

Raundi imeanza kwa kasi lakini baadaye kila bondia ameonekana kutegea na kumspma mwenzake

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic