April 25, 2017



Mashabiki wa Yanga wameanza kuonyesha mwamko kuichangia klabu yao baada ya ombi la uongozi kuwaomba wafanye hivyo.

Hata hivyo, uongozi huo umesema kila baada ya wiki utakuwa utakuwa ukitoa taarifa kuelezea kinachoendelea.

Ifuatayo ni taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, leo.

TAARIFA KWA UMMA:
Klabu ya soka ya Yanga SC kupitia Katibu Mkuu Charles Boniphace Mkwasa inashukuru sana kwani zoezi la uchangiaji toka kwa wanachama limekuwa zuri na likiendelea vyema.

Pia uongozi utakuwa ukitoa taarifa ya makusanyo kwa wanachama wake kila baada ya wiki moja ili waweze kufahamu mwenendo wa michango yao kwa klabu.

Klabu ina thamini mtu wa kipato chochote kuichangia klabu na kwa chochote unachotoa klabu inatanguliza shukrani za dhati na kutambua umuhimu wako katika mchakato huu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano; 
Young Africans SC

25/04/2017

1 COMMENTS:

  1. Naombeni namba ya Katibu wa timu yangu ya Yanga ndugu Bonifasi Mkwasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic