April 29, 2017


MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MANJI


TAARIFA KWA UMMA 
Ninayo furaha kuwatangazia wanachama , wapenzi , mashabiki na wadau wa Yanga SC kuhusu makusanyo ya fedha za maendeleo ya klabu kutoka kwenu kwa akaunti maalumu ya Selcom namba 150334. 

Makusanyo haya yanafanyika kupitia mitandao ya Mpesa , Tigo Pesa na Airtel Money . Hakika mpaka sasa mwitikio ni mzuri na mimi kama katibu mkuu sambamba na jopo zima la uongozi tunawashukuru sana wanachama wetu kwa moyo huu mkubwa kwa timu yenu . Hakika tunajivunia ushirikiano wenu na tunawaomba taarifa ya leo iwe chachu ya kufanya kikubwa zaidi ya hiki. 

Ripoti yetu inaanzia siku ya kwanza ya tarehe 24 April 2017 saa saba mchana ( 13:00hrs ) tulipozindua harambee hii mpaka  tarehe 27 April 2017 saa 7 mchana ( 13: 00 Hrs ) . 

Makusanyo ;
1.24 April 2017 tulipokea entries 642 na jumla ya makusanyo ikawa 2 ,184,911.00

2. 25 April 2017 tulipokea entries 1181 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 4, 248,751.00

3. 26 April 2017 tulipokea entries 625 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 2,296,966.00

4. 27 April 2017 tulipokea entries 290 na jumla ya makusanyo ikawa Tsh 866,795.00

Jumla ya entries tulizopokea ni 2738 na kukusanya kiasi cha fedha cha Tsh milions 9 597 423.00/-

Mungu awabariki sana . Kama uongozi tunasisitiza fedha hizi zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa baada ya kukusanywa . Lakini angalizo kwetu ; ukiangalia tarehe na entries ( wachangiaji ) toka siku ya kwanza mpaka jana inakwenda inashuka . Hii ina maana kwa kiasi fulani hamasa yetu inapungua . 

Tunawaomba kwa pamoja tuhamasishane kupandisha makusanyo haya badala ya kushuka . Kama tulivyochangia siku ya tarehe 25 April kiasi cha shilingi milioni 4 basi tusishuke chini ya hapo . 

Mwisho binafsi Boniface Mkwasa kama katibu mkuu wa klabu kwa niaba ya uongozi tunawashukuru na kuwaomba ripoti hii iwe chachu ya kuchangia zaidi ili juma lijalo nikitoa taarifa iwe zaidi ya hii. Kwa siku tatu kukusanya shilingi milioni 9! toka kwenu hakika ni jambo kubwa.

Imetolewa na Idara ya habari na mawasiliano
Young african Sports Club

28.04.2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic