April 15, 2017

MBAO FC

Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Mbao FC dhidi ya  Tanzania Prison kesho, sasa itachezwa kwenye uwanja usio na majukwaa wa Nyamgana ambao uko katikati ya jiji la Mwanza.

Imeelezwa katika uwanja wa CCM Kirumba kuna matamasha ambayo yamelazimu mchezo huo kuhamishwa.

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mwanza (MZFA), Leonard Malongo amesema imelazimika kuwa hivyo.

“Hatuna ujanja, sasa hii mechi ya kesho Jumapili itachezwa Nyamagana,” alisema.


Kama ni hivyo, maana yake Mbao FC na Prisons zinaandika rekodi ya kuwa timu za kwanza kucheza katika uwanja huo tokea uwekewe nyasi bandia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic