April 29, 2017

MKEMI (KULIA)


Na Saleh Ally
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzajia (TFF) imetangaza kumuita mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi.

Mkemi ameitwa kujieleza kuhusiana na suala la kuishambulia TFF na kamati zake. Hapa kitakachofanyika ni kumfungia Mkemi, hakuna ziada.

Mkemi ameonekana aliidhalilisha TFF na kamati zake wakati Kamati ya Saa 72 ilikuwa inajiandaa kusikiliza rufaa ya Simba kwa Kagera Sugar.

Alieleza namna ambavyo Simba hawakustahili kupewa pointi tatu huku akionyesha kuwa na hofu au figisu ndani ya kamati na shirikisho hilo kwamba walipanga kuipa Simba pointi tatu na mabao matatu.

Baada ya hapo, kamati ilikaa na kutoa uamuzi wa kuipa Simba pointi tatu. Hakukuwa na kesi yoyote iliyimuhusu Mkemi.

Msemaji wa Simba, Haji Manara naye akaanza kutupa lawama zake TFF na inaelezwa baada ya kuwa na taarifa kwamba kulikuwa na figisu za kurudisha pointi za Kagera.

Hii ilionekana ni matakwa binafsi kwa kuwa kadi tatu zilibainika. Tulijua TFF ambao ni watunza rekodi watabainisha hilo.

Mfano wakiipa Simba iendelee kubaki na pointi tatu, wataeleza namna kadi tatu zilivyopatikana. Kama wataamua kuirudishia Kagera, basi wataeleza pia.

Wao wakarudisha pointi kwa Kagera na hawakusema lolote kuhusiana na kadi tatu, badala yake walizungumzia suala la uhalali wa rufaa ya Simba, kwamba ilichelewa na kadhalika.

Hiyo bado halikuwa jibu sahihi kwa kuwa hata kama Simba wasingekata rufaa na kungekuwa na kadi tatu, basi TFF ndiyo walipaswa kuipoka Kagera pointi.

MANARA

Bado hadi leo hawajataja lolote kama ni kadi mbili au tatu. Kwa aibu au kiburi wameendelea kunyamaza na hawataki kuulizwa, wanaendelea kuonyesha ni wasiojali.

Malalamiko ya uonevu wa adhabu aliyopewa Manara, yanaonekana kuanza kuwatafuna TFF kwa kuwa kumfungia miezi 12 na faini ya Sh milioni 9 ni uonevu wa wazi ambao unaonyesha ni mlengo wa kukomoana na kanuni za uendeshaji ligi ni zile zilizo kwa ajili ya kuwakomoa wadau wa soka na kuwalinda mabwana ambao wanalifanya shirikisho hilo kama lao.

Kuitwa kwa Mkemi, ni kutaka kupoza ambacho TFF wanaamini si sawa, si haki na upungufu wa usahihi ambao wameufanya.

JIULIZE….kwanini walianza kumuita Manara na wakampa adhabu kabla ya Mkemi?

JIULIZE….vipi wasikie watu wanalalamika ndiyo wakamuita Mkemi?

NAKUHAKIKISHIA….Mkemi atafungiwa tu, baada ya hapo Simba wanaolalamika, sasa Yanga wataanza kulalamika na TFF watatengeneza muonekano wa “tunatenda haki kote”.

TFF inaonekana haina watu wataalamu ubunifu wa mipango thabiti kwenye wakati mgumu kwa kuwa mingi wanayopanga inawaangusha.

Kumuita Mkemi kipindi hiki ni kuzidi kuonyesha udhaifu wa hali ya juu ambao unathibitisha wao wanaweza kufanya mambo kwa mihemko au kusukumwa na kauli au malalamiko tu ya watu.

MWISHO JIULIZE…walimsahau Mkemi? Hawakuumizwa na kauliza zake awali? Nani aliwakumbusha kuwa amesema lugha ambazo si sahihi? Pia, kwanini walianza kuona Manara amekosea kabla ya Mkemi?

Tunapokwenda, TFF tuliyonayo itatuangusha na tutabaki kujivunia kitu kimoja tu, Serengeti Boys ambayo ni mwanzo mzuri wa kazi ya Leodeger Tenga ambaye aliacha msingi mzuri na umeendelea kuvurugwa na uongozi unaofanya mambo ili mradi wa TFF ya sasa.


FIN.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic