April 29, 2017




Azam FC ina furaha baada ya kurejea uwanjani kwa straika wake John Bocco, lakini Simba imesema hata kama mchezaji huyo atacheza leo dhidi yao, ni lazima wao washinde.


Bocco alikuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza majeraha ya nyama za paja na ndiye aliyeifungia Azam dhidi ya Simba katika ushindi wa bao 1-0 wa timu yake katika Ligi Kuu Bara Januari 28, mwaka huu. Simba pia ilifungwa bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu.


Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba inacheza na Azam mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA ambapo mshindi atacheza fainali ya michuano hiyo.


Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema wanathamini mchango wa Bocco kwa timu yake lakini watapambana ili washinde mchezo huo.


“Najua Azam wanategemea nafasi hii pekee ili wacheze Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, hawa tunawafunga na hawatacheza mechi za kimataifa mwakani, hii ni nafasi yetu.


“Hawatapanda ndege msimu ujao kwani tunataka kuwabania nafasi hii ya FA wanayoitaka na tunataka kulipa kisasi kwani Azam wametufunga mara mbili mwaka huu,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic