April 23, 2017



Hafla maalumu inayohusisha droo ya upangaji wa ratiba hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.


Hafla hiyo itahusisha droo ya timu nne zilizovuka katika hatua ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


Timu nne zilizofuzu ni Simba, Azam FC, Mbao FC ya Mwanza na Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi na hii kuna uwezekano mkubwa watani wa jadi Yanga na Simba kukutana katika hatua ya nusu fainali.

Msimu uliopita Simba waling’olewa na Coastal Union kwenye robo fainali na kukutana na Yanga kwenye hatua ya nusu fainali ambayo ilishinda na kwenda fainali ilipokutana na Azam.

Katika upangaji, hakuna uhakika nani atakutana na nani na kwa kuwa timu ni nne, maana yake kutakuwa na vyungu viwili tu vya timu mbili kila upande.


Yanga na Simba, kukutana ni rahisi sana na inawezekana hilo litatokea na kuzua ushindani mpya wa watani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic