May 3, 2017

SHINDA NYUMBA WASHINDI wanne wa droo ndogo ya tatu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili iliyofanyika wiki iliyopita katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam, wamekabidhiwa zawadi zao leo katika hafla liyofanyika kwenye ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge mapema leo.
Mgaza Mwemanga wa Manzese jijini Dar akipokea zawadi ya smartphone (Tecno Phantom6) kutoka kwa mwakilishi wa TECNO
Katika makabidhiano ya zawadi hizo, Ofisa Uhusiano wa Global Publishers, Soud Kivea, aliwataja washindi kuwa ni Agnes Lyimo wa Tanga aliyejishindia zawadi ya pikipiki (imechukuliwa kwa niaba yake na shemeji yake, Juma Ahmad); Mgaza Mwemanga wa Manzese jijini Dar aliyejishindia simu ya kisasa aina ya Phantom 6, Shaban Muhindila wa Morogoro aliyepata Seti ya Televisheni (Flat Screen) na Aveline Thomas wa Keko jijini Dar (Dinner Set).
Mr. Shinda Nyumba akimkabidhi Juma Ahmad zawadi ya begi kwa niaba ya dada yake Agnes Lyimo aliyejishindia pikipiki.
Juma Ahmad akikabidhiwa kadi ya pikipiki.
“Tunawasihi wasomaji wa magazeti yetu ya Championi, Ijumaa, Amani, Risasi, Uwazi na Ijumaa Wikienda waendelee kukata kuponi zao kwa sababu zawadi zingine bado zipo za kutosha kabla ya bahati nasibu kubwa kwa ajili ya nyumba ambayo ipo Dar es Salaam,” alisema Kivea.
Mwakilishi kutoka British School akikabidhi zawadi ya dinner set kwa Jonathan Chingwile aliyefika kumpokelea ndugu yake, Everyne Thomas.
Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology ambao wawakilishi wao pia walikuwepo katika hafla hiyo na kupata fursa ya kuwaelezea wananchi juu ya ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa. Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Kivea amesema kuwa ili mtu aweze kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba, anachotakiwa kufanya ni kununua Magazeti ya Global Publishers ambayo ni Amani, Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko na Uwazi kisha kujaza kuponi iliyoko ukurasa wa pili wa kila gazeti yaliyotajwa hapo juu, baada ya hapo mshiriki atakata kuponi na kuituma Global Publishers ama kwa wakala aliye karibu naye kama maelekezo yanavyoonekana kwenye kuponi hiyo.
Juma Ahmad akipanda kwenye pikipiki aliyokabidhiwa.
Baada ya hapo mshiriki atakuwa yuko kwenye nafasi ya kushindania vitu mbalimbali vikiwemo TV Flat Screen, Simu aina ya smart phones, dinner set, king'amuzi cha Tin pamoja na zawadi kubwa kabisa ya NYUMBA NA FENICHA ZAKE itakayotolewa kwenye droo ya kubwa.
Washindi katika picha ya pamoja.
Washindi pamoja na timu ya Shinda Nyumba ya Global TV wakiwa katika picha ya pamoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic