May 25, 2017




Baada ya taarifa kwamba John Bocco amesaini Simba miaka miwili. Taarifa nyingine za uhakika zimeeleza, Simba wanakutana leo usiku kujadili suala hilo.

Taarifa zinasema, Kamati ya Usajili ya Simba itakutana leo usiku baada ya saa za kazi kujadili suala hilo.

"Suala la Bocco lipo, lakini kama ni mkataba basi wa awali. Lakini kusema saini kabisa hadi sasa hakuna," kilieleza chanzo cha uhakika kutoka Simba.

"Tunakutana leo usiku na masuala ya usajili yatajadiliwa nasi ndiyo tutatoa jambo, nafikiri hiyo sasa itakuwa kesho."

Taarifa za Bocco kutua Simba zimeonekana kuwashitua watu wengi ingawa imeelezwa kama ni mkataba, basi ni ule wa awali.

Lakini kumekuwa na taarifa kwamba Azam FC imeamka baada ya taarifa hizo na kuna juhudi zinafanyika kutaka kurekebisha mambo ili nahodha wao abaki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic