May 13, 2017Kocha wa timu ya taifa vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime amesema watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya Mali  katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Port Gentil, Gabon.


Serengeti imepangwa Kundi B sambamba na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali, Niger na Angola na inahitaji kushinda michezo miwili ili iweze kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika mwaka huu nchini India.


Akizungumza kutoka Gabon, Shime alisema kikosi chake kipo tayari kuingia vitani katika michuano hiyo kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya hivyo ana imani kubwa watashinda mchezo huo.


 “Tunashukuru kila kitu kinaenda vizuri hakuna mchezaji yeyote majeruhi tunachosubiria ni kuanza kwa michuano, naamini mechi saba tulizocheza za kirafiki zimetoa mwanga mkubwa kwa uelekeo wa timu yetu katika michuano hii.

 “Hatuwezi kuwahofia Mali kwa sababu moja kati ya timu ambazo zinatajwa kuwa ni ngumu Serengeti Boys ipo, kikubwa ambacho tumekifanya ni kuwaondoa woga vijana wetu.

“Tumewaongezea hali ya kujiamini kwa sababu hii ndiyo michuano tuliyokuwa tunaipigania kupata nafasi, naamini kwamba Mali tutawafunga kikubwa Watanzania waendelee kutuombea,” alisema  Shime.

MECHI ZA SERENGETI
Jumatatu Mali v Serengeti
Mei 18, Serengeti v Angola

Mei 21, Serengeti v Niger

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV