May 13, 2017



Amissi Tambwe wa Yanga amesema kwa jinsi mambo yanavyokwenda, ana uhakika asilimia 100 mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara atatokea katika timu yake.

Tambwe amesema anapata nguvu ya kutoa kauli hiyo kutokana na ukweli kwamba, katika kikosi chao ndipo wanapotokea wachezaji wengi wanaojua kufunga.

Simon Msuva wa Yanga ana mabao 13 akifuatiwa na straika wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa mwenye mabao 12.

Obrey Chirwa wa Yanga, Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar) na Shiza Kichuya wa Simba wote wana mabao 11 na Tambwe mwenyewe anayo kumi.

Tambwe amesema kwa aina ya uchezaji ya Yanga hadi sasa unaifanya safu yao ya ushambuliaji kuwa tishio kutokana na kila mmoja kumtengenezea mwenzake nafasi ya kufunga pale anapopata nafasi.

Tambwe alisema, kwenye tano bora ya wafungaji katika orodha ya wafungaji inatawaliwa na wachezaji wa Yanga ambao wamefunga idadi kubwa ya mabao.

Aliongeza kuwa, katika kufanikisha hilo wanamtoa mfungaji bora, wamepanga kucheza mechi zote zilizobakia kwa ushirikiano bila ya kunyimana pasi kwenye safu yao ya ushambuliaji.

“Hadi hivi sasa ni uhakika kuwa mfungaji bora wa msimu huu anatoka Yanga, hili halina ubishi na wala halihitaji kubishana na mtu, kikubwa kama kuna ambaye anaweza kubisha asuburie hadi mwisho aone.

“Pia tuna michezo mingi kuliko timu nyingine, hivyo nafasi ya kuchukua ufungaji bora ipo kwetu kwa sababu nyingi,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic